-
Je, tunakwenda wapi tunapokufa? (Where do we go when we die?)
Je, tunakwenda wapi tunapokufa? Ninadhani hili ni swali ambalo kila mtu aliyewahi kuishi amewahi kulifikiria, kwa sababu Kifo ni kitu ambacho kila mmoja wetu atakabiliana nacho. Kwa kadiri tunavyokuwa na kukomaa, tunawaona wale wanaotuzunguka wakifariki. Na ukweli uko wazi kabisa kwamba hata sisi siku moja tutakufa na huwa tunajiuliza ni nini kitafuata baadaye? Unajua kuwa kuna dhana nyingi zilizotolewa ili kulijibu hili swali. Lakini unajua kama mkristo, sipaswi kujiingiza kwenye mchezo wa kubashiri. Sipaswi kukubaliana na mambo ya uchawi au hadithi za uongo, kwa sababu ninaweza kulijua jibu la swali langu, si tu Je, ni wapi nilipotokea, lakini pia Je, ninakwenda wapi. Katika somo hili tutakwenda kuiangalia safari ya roho ya mwanadamu na tutaiacha Biblia itujibie, Je, tunakwenda wapi tunapokufa?
-
Ukweli Kuhusu Mbinguni (The Truth About Heaven)
“Je, mbinguni ni mahali halisi?” Labda unaiangalia video hii, na pengine unafikiria, “Mimi siamini uwepo wa mbingu. Si lolote ni mashaka tu!” Niruhusu ni kueleze kwamba, “Ndiyo, mbinguni ni mahali halisi.” Je, nimelijuaje hilo? Vyema, si kwa sababu ya uzoefu binafsi. Sijawahi kufika huko. Imani ya mtu kuhusu uwepo wa mbingu inategemea kwanza kwenye uthibitisho wa uwepo wa Mungu, na pili kwenye kutokuwapo na makosa katika Biblia.
-
Ukweli Kuhusu Jehanum (The Truth About Hell)
Unajua, kuna uelewa mbovu sana kuhusu Jehanamu. Kwa baadhi ya watu, uelewa wao kuhusu Jehanamu auendi mbali zaidi ya vikaragosi ambavyo walikuwa waikiviangalia walipokuwa watoto. Wanaifikiria Jehanamu kama vile ni nyumba ya shetani, Ambako anakaa akiwa na chungu cha moto kinachochemka na uma. Watu wengine wanafikiri “Jehanamu ni neno la kawaida tu ambalo linatumiwa kwa lugha ya mfano katika Biblia. Bado wengine wanaifikiria Jehanamu kama sehemu ya maumivu ya muda mfupi halafu mtu anaungua na kutoweka kabisa. Kwa hivyo kulingana na kutokuelewa huku, hebu tujibu hili swali, “Je,Jehanamu ni nini?”
Je, tunakwenda wapi tunapokufa? (Where do we go when we die?)
Description