Je, tunakwenda wapi tunapokufa? (Where do we go when we die?) | WVBS Online Video

Je, tunakwenda wapi tunapokufa? (Where do we go when we die?) Program


Je, tunakwenda wapi tunapokufa? Ninadhani hili ni swali ambalo kila mtu aliyewahi kuishi amewahi kulifikiria, kwa sababu Kifo ni kitu ambacho kila mmoja wetu atakabiliana nacho. Kwa kadiri tunavyokuwa na kukomaa, tunawaona wale wanaotuzunguka wakifariki. Na ukweli uko wazi kabisa kwamba hata sisi siku moja tutakufa na huwa tunajiuliza ni nini kitafuata baadaye? Unajua kuwa kuna dhana nyingi zilizotolewa ili kulijibu hili swali. Lakini unajua kama mkristo, sipaswi kujiingiza kwenye mchezo wa kubashiri. Sipaswi kukubaliana na mambo ya uchawi au hadithi za uongo, kwa sababu ninaweza kulijua jibu la swali langu, si tu Je, ni wapi nilipotokea, lakini pia Je, ninakwenda wapi. Katika somo hili tutakwenda kuiangalia safari ya roho ya mwanadamu na tutaiacha Biblia itujibie, Je, tunakwenda wapi tunapokufa?

From Series: Language: SwahiliVideos in this Program

© 2025 WVBS Online Video